WADAU WA MAENDELEO WAKUTANA NA MENEJIMENTI YA TASAF

User Rating: 0 / 5

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Wadau wa Maendeleo na menejimenti ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- wamekutana jijini DSM kwenye Ofisi Ndogo za Mfuko huo Kujadili pamoja na mambo mengine maandalizi ya zoezi la kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini litakalofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao.

Utaratibu huo wa kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini hufanyika mara mbili kwa mwaka na hujumuisha Maafisa wa Serikali  na wadau wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi ambao hupata fursa ya kutembelea baadhi ya maeneo na kukutana na Walengwa na Viongozi wa Maeneo ya Utekelezaji wa Mpango.

Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF imekuwa ikitekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini –PSSN- ulioanza mwaka 2012 katika baadhi ya Halmashauri za Wilaya kwa majaribio na kisha kutekelezwa nchini kote kufuatia mafanikio ya majaribio yaliyofanyika katika wilaya za Bagamoyo, Kibaha, Chamwino na Mbarali mkoani Mbeya.

Kwa sasa Mpango huo unanufaisha Kaya takribani Milioni Moja na Laki Moja Tanzania Bara ,Unguja na Pemba ambako walengwa hupata ruzuku ya Masharti hususani katika nyanja za elimu na afya na ile isiyokuwa ya Masharti kwa lengo la kuboresha maisha ya walengwa .

Kufuatia utekelezaji wa Mpango huo wa Kunusuru Kaya Maskini, Walengwa wa Mpango huo wameonyesha mabadiliko makubwa hususani katika uboresha ya makazi ,uanzishaji wa miradi ya kiuchumi  huku suala la mahudhurio ya wanafunzi wanaotoka kwenye Kaya hizo shuleni na kwenye vituo vya afya yakiboreshwa zaidi.

Serikali kupitia TASAF kwa sasa iko katika maandalizi ya Awamu ya Pili ya utekelezaji wa Mpango huo ambayo mkazo maalum utawekwa kwa Walengwa kufanya kazi na kuibua miradi itakayowaondolea kero kwa kushirikiana na Wataalamu walioko kwenye maeneo yao huku pia mkazo mkubwa ukiwekwa kwenye shughuli za uzalishaji mali ili waweze kukuza uchumi wao na hivyo kupunguza umaskini.

 pic1

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw.Ladislaus Mwamanga (katikati) akimsikiliza kiongozi wa Shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia Bw. Mohamed Muderis (mwenye miwani)

pic2

Wadau wa Maendeleo na Menejimenti ya TASAF (picha ya juu na chini wakiwa katika mkutano wa kujadili utekelezaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini jijini DSM.

pic3

pic4

pic5

Menejimenti ya TASAF wakiwa katika mkutano na Wadau wa Maendeleo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mfuko huo kujadili masuala ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo jijini DSM.

MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA, DR. HAFEZ GHANEM AVUTIWA NA MAFANIKIO YA SERIKALI KATIKA KUPAMBANA NA UMASKINI KUPITIA TASAF.

User Rating: 0 / 5

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika,Dr. Hafez Ghanem amefanya ziara katika mtaa wa Mamboleo,halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini DSM na kukutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.

Akizungumza na Walengwa hao baada ya kukagua bidhaa wanazozitengeneza kama njia mojawapo ya kukuza kipato chao, Dr. Ghanem amesema jitihada waliyonyesha Walengwa hao ya kuuchukia Umaskini ,itaendelea kuungawa mkono na Benki hiyo ya Dunia ambayo amesema ni rafiki mkubwa wa Serikali ya Tanzania.

Dr.Ghanem ametoa rai maalum kwa Walengwa hao wa TASAF kutumia fursa hiyo kuongeza uzalishaji mali na kutumia mazingira mazuri ya kujiletea maendeleo kwani amesema ni dhahiri kuwa serikali ya Tanzania inawajali na imeonyesha utayari wa kuboresha maisha ya wananchi.

Aidha Makamu huyo wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika ambaye aliambatana na Mkurugenzi Mkazi wa  Benki hiyo Bi. Bella Bird, amesisitiza kuwa taasisi hiyo kubwa ya fedha Duniani itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kufadhili Mpango huo wa Kunusuru Kaya Maskini kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha utekelezaji wake.

Akizungumza kwenye Mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga ameelezea mafanikio makubwa ambayo Mfuko huo umepata tangu kuanzishwa kwake takribani miaka 18 iliyopita hususani katika nyanja za elimu,afya,maji, na uchumi.

Bw. Mwamanga amesema mafanikio makubwa yaliyopatikana yametokana pia na usimamizi wa Karibu wa viongozi wa Serikali katika ngazi zote za utekelezaji ambapo wamekuwa wakiwahamasisha wananchi kutumia vizuri fursa hiyo ili waweze kuinua kiwango chao cha maisha na kutokomeza umaskini kwa kasi kubwa zaidi.

Benki ya Dunia pamoja na taasisi nyingine za Kimataifa imekuwa ikichangia fedha kugharamia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao kwa sasa unahudumia takribani kaya Milioni Moja na Laki Moja Tanzania Bara, Unguja na Pemba,Mpango ambao umekuwa chachu ya maendeleo kwa Kaya za Walengwa.

 pic1

Makamu Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika,Dr.Hafez Ghanem,akivishwa skafu alipowasili kwenye mtaa wa Mamboleo,wilayani Temeke jijini DSMalipokutana na Walengwa wa TASAF.

pic2

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Dr. Hafez Ghanem akiwa katika picha ya pamoja na  baadhi ya wanafunzi ambao wazazi wao wako katika Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na serikali kupitia TASAF.

pic3

Baadhi ya walengwa wa TASAF wa Mtaa wa Mamboleo-Temeke jijini DSM wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa WB kanda ya Afrika Dr. Hafez Ghanem na viongozi wengine akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga kulia kwa Makamu huyo wa Rais wa WB.

pic4

pic5

 

WALENGWA WA TASAF WAFURAHIA MAONYESHO YA SIDO MKOANI SIMIYU.

User Rating: 0 / 5

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF waliopata fursa ya kushiriki katika maonyesho yaliyoandaliwa na Shirika la Kuhudumia viwanda vidogo vidogo –SIDO yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu wamesema maonyesho hao yamekuwa ya manufaa makubwa kwao na kuishukuru serikali kupitia TASAF kwa kuwawezesha .

Maonyesho hayo yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassimu Majaliwa yanawashirikiwa Wajasiliamali wadogo na wakati ambao wamepata fursa ya kuonyesha bidhaa wanazozalisha na pia kujifunza teknolojia rahisi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa lengo la kutimiza azma ya serikali ya kukuza sekta ya viwanda nchini.

Bidhaa zilizoletwa na Walengwa wa TASAF kwenye maonyesho hayo hutengenezwa kwa njia ya vikundi baada ya kuwezeshwa na Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii kama njia mojawapo ya kuinua kipato cha Walengwa na kupunguza adha ya umaskini.

Miongoni mwa bidhaa ambazo Walengwa hao wa TASAF wanaonyesha , ni pamoja na sabuni za vipande na maji, majani ya chai yaliyozalishwa kutokana na mmea wa mchaichai,vyungu,bidhaa za ususi ,nguo aina ya batiki,urembo na mafuta ya kupakaa.

Wakizungumza kwenye banda hilo la TASAF, Walengwa hao wamesema fursa waliyoipata imewawezesha siyo tu kuuza na kupata soko la bidhaa zao, bali pia wameweza kujifunza mbinu za kuendesha shughuli za uzalishaji mali wenye tija jambo ambalo wamesema litainua kipato chao.

“Tunashukuru sana TASAF kwa kutufungua macho tumeweza kujua namna bora ya kuendesha shughuli zetu za kuzalisha bidhaa na kupata soko “amesema mmoja wa Walengwa ambaye kikundi chake kinajishughulisha na uzalishaji wa mafuta ya kujipakaa na sabuni.

Wakizungumzia changamoto wanayokabiliana nayo katika utekelezaji wa shughuli za uzalishaji wa bidhaa zao, Walengwa hao wametaja tatizo la uduni wa vifungashio vya bidhaa ambayo wamesema ikipatiwa ufunguzi watakuwa wamepiga hatua kubwa kuelekea katika maendeleo ya uhakika.

“Tazama hivi sasa tunalazimika kuweka sabuni ya maji kwenye chupa za plastiki tunazookoteza baada ya kutumika na kutupwa na watumiaji wengine jambo hilo linapunguza sana ubora wa bidhaa zetu” amelalamika mlengwa huyo wa TASAF.

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umekuwa na utaratibu wa kuwashirikisha baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko huo kwenye maonyesho mbalimbali ya Wajasiliamali ili kuwawezesha Walengwa hao kujifunza na kuonyesha bidhaa wanazozalisha kwa lengo la kupata pia soko la bidhaa zao.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za Walengwa na Maafisa wa TASAF wakiwa kwenye maonyesho hayo.

pic1

 

pic2

 

pic4

 

pic3