Karibu
Ndg. Shedrack S. Mziray
Mkurugenzi Mtendaji
Kwa niaba ya Uongozi na Wafanyakazi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), ninakukaribisha kwa moyo wa dhati kwenye tovuti yetu rasmi. Hapa utapata nafasi ya kujifunza, kuchunguza na kushiriki katika kazi tunazofanya kubadilisha hali za maisha ya walengwa pamoja na jamii kwa ujumla.
Dhamira yetu ya kupunguza umaskini na kuchochea maendeleo endelevu inaonekana kupitia shuhuda za kusisimua na mafanikio tuliyoyapata. Tunapokaribia kufikia mwisho wa Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN II) ifikapo Septemba 2025, tunajivunia mamfanikio makubwa ambayo yamebadili kwa kiasi kikubwa maisha ya maelfu ya watu nchini kote.
Kupitia Ajira za Muda, Uhawilishaji wa Fedha na Kuendeleza Vikundi vya Kijamii vya Kuweka Akiba na Uwekezaji (COMSIP) - TASAF, kwa ushirikiano wa karibu na asasi za Serikali, washirika wa maendeleo na wadau mbalimbali, imepata mafanikio makubwa. Kwa pamoja, tumewezesha kupunguza kiwango cha umaskini, kuongeza idadi ya watoto wanaojiunga na shule na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya, pamoja na mafanikio mengine mengi. Tathmini ya hivi karibuni iliyofanywa na wataalamu wa mazingira kutoka Benki ya Dunia imebainisha matokeo chanya ya kazi za TASAF.
Tathmini hiyo ilibainisha mafanikio yetu na kuonesha maeneo yanayohitaji kuboreshwa; na hivyo kutuwezesha kuboresha zaidi kazi zetu katika kuhudumia jamii. Kupitia miradi yetu - Ajira za Muda, Uhawilishaji wa Fedha, na Vikundi vya Kuweka Akiba na Kuwekeza - TASAF, kwa ushirikiano wa karibu na asasi za Serikali, Wadau wa Maendeleo, na wadau wengine, imepiga hatua kubwa katika kuboresha miundombinu ya jamii na kuboresha maisha.
Miradi hii sio tu imetoa fursa za ajira, bali pia imepunguza kiwango cha umaskini, kuongeza idadi ya watoto wanaojiunga na shule na kuboresha upatikanaji wa huduma muhimu za afya kwa kaya maskini nchini kote. Juhudi hizi zinaonesha dhamira ya TASAF ya kukuza maendeleo endelevu na kuboresha ubora wa maisha kwa makundi yaliyo hatarini kote nchini. Tunapotafakari safari yetu, tunajivunia kuboreka kwa uchumi wa kaya zinazonufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. Utekelezaji mzuri wa mpango huu umebadili kabisa hali ya kiuchumi ya takribani kaya 1,400,000 na wanakaya takriban milioni 5.5 kwa kuwapa uwezo wa kujitegemea na kushiriki katika shughuli za kuongeza kipato.
Tunakushukuru kwa kuwa sehemu muhimu ya safari yetu.
Shedrack S. Mziray
Mkurugenzi Mtendaji