Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

Washirika wa Maendeleo wafurahishwa na mafanikio ya Walengwa Manispaa ya Bukoba


Kiongozi wa wajumbe wa Mkutano wa Mapitio ya Pamoja ya utekelezaji wa Mpango wa TASAF waliotembelea Manispaa ya Bukoba Ndg.Paulina Mrosso akizingumza na walengwa wa Mpango wa Kusurusu Kaya Maskini katika mtaa wa Kalabekangaiza Manispaa ya Bukoba. Kushoto kwake ni Mratibu wa TASAF Mkoa wa Kagera Ndg. Efrazi Mkama na Kaimu Mkurugenzi wa Mifumo, Tathmni na Ufuatiliaji wa TASAF Ndg. Peter Lwanda

Wajumbe wa Mkutano wa Mapitio ya Pamoja ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wameonesha kuridhishwa na utekelezaji wa  Awamu ya Pili ya Mpango katika Mamlaka ya Eneo la Utekekezaji la Manispaa ya Bukoba.

Kiongozi wa Ujumbe huo Ndg. Paulina Mrosso kutoka Benki ya Dunia amesema hayo baada ya kuhitimisha ziara ya mapitio ya pamoja baina ya Serikali na Washirika wa Maendeleo kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa katika Manispaa ya Bukoba.

Ujumbe wa ziara hiyo uliambatana na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais- Ikulu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Ubalozi wa Norway pamoja na watumishi wa TASAF.

“Miongoni mwa mambo tuliyoyaona wakati wa ziara yetu hapa Bukoba ni kwamba Mpango unafahamika vizuri kwa walengwa na pia taarifa tulizopewa hapa ofisini zinaendana na uhalisia uliopo kwa walengwa,” alisema.

 “Pia  tumeona utekelezaji mzuri wa  afua zote za Mpango  zilizopelekea walengwa kukidhi vigezo vya kwenye ruzuku ya masharti lakini pia  tumeona  jinsi  afua ya  kuinua uchumi wa kaya inavotelezwa kwa ufasaha,” alisema.

Bi. Paulina alisema, utekelezaji wa afua ya kuinua uchumi wa kaya, walengwa wamekuwa wakipewa elimu ya kuweka akiba na kukopeshana na hivyo kuwafanya

Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Mtaa wa Kabalekangaiza  Manispaa ya Bukoba  waliohudhuria mkutano wa Wajumbe wa Mkutano wa Mapitio ya Pamoja ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

Kauli ya Bi. Paulina iliungwa mkono na Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Norway Bw. Priva Clemence ambaye aliwahimiza walengwa kutumia vizuri ruzuku yao ili wawe na kipato kitachowawezesha kumudu gharama za maisha pindi mradi utakapofikia tamati.

Kaimu Mkurugenzi wa Mifumo, Ufuatiliaji na Tathmini wa TASAF Bw. Peter Lwanda alisisitiza dhamira ya Mfuko kuendelea kuhudumia walengwa wa kaya maskini ili ziondokane na hali duni.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Pojestus Lubanzibwa alishukuru Serikali na Washirika wa Maendeleo kwa kusaidia kuinua uchumi wa kaya maskini na kwamba hatua hiyo imechangia kupunguza hali ya utegemezi.