Habari
TAARIFA MUHIMU
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) unapenda kuutangazia umma kuwa, HAUJATOA TANGAZO LA NAFAZI HIZI ZA KAZI ZINAZOSAMBAA KWENYE BAADHI YA MITANDAO YA KIJAMII.

Mfuko unaomba jamii ipuuze taarifa za tangazo hilo ambalo tunaamini linasambazwa kwa nia ovu.
Tunapenda kukumbusha umma kuwa Matangazo, taarifa na habari za Mfuko TASAF hutolewa kwenye njia rasmi za mawasiliano ikiwemo anuani za mitandao zifuatazo:
✔️ Mitandao ya Kijami: Instagram, Facebook, na X (@tasaf.tanzania)
✔️ Tovuti: www.tasaf.go.tz
Tafadhali hakikisha habari unazozipata ni sahihi kabla ya kuchukua hatua.
