Kuimarisha Mifumo ya Taasisi
Uimarishaji wa mifumo unahakikisha kuna uwezo wa kutosha wa watendaji katika ngazi za mamlaka za eneo la utekelezaji na mikoa. Pia wadau wengine katika ngazi za Taifa zikiwemo Wizara na idara za Serikali ambazo zinafanya kazi moja kwa moja na Mpango, zinapata elimu na uelewa wa kutosha kuhusu taratibu za utekelezaji wa Mpango, masuala ya fedha na manunuzi, ushiriki wa jamii katika shughuli za kuongeza kipato, kusimamia utekelezaji na kutoa ushauri kwa jamii wakati wa utekelezaji wa shughuli za Mpango.