Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini - Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu
Kipindi cha Pili cha TASAF Awamu ya Tatu ni cha miaka minne kuanzia 2020 hadi 2023. Kipindi hiki kinatekelezwa katika Mamlaka za Utekelezaji 187, ambazo ni Halmashauri zote za Tanzania Bara, Unguja na Pemba. Mpango unatekelezwa katika Vijiji/Mitaa/Shehia zote nchini. Walengwa wa Mpango katika kipindi hiki ni kaya zaidi ya 1,4000 zenye watu wanaokadiriwa kufikia 7,000,000.
Madhumuni ya Kipindi cha Pili ni kuongeza fursa za kujiongezea kipato na kuboresha huduma za kiuchumi na kijamii kwa kaya za walengwa na kulinda maslahi ya watoto wao.
Kipindi cha Pili kitafikia malengo yake kwa kutekeleza shughuli mbalimbali kupitia sehemu kuu tatu ambazo ni uhawilishaji fedha ambao utaongeza kipato cha kaya na kuwekeza katika afya na elimu ya watoto, kuinua uchumi wa kaya kwa kujenga uwezo kwa kaya katika utunzaji rasilimali na kutengeneza njia mbadala na endelevu za ajira na kushiriki katika kazi za jamii na kupata kipato cha ziada kwa matumizi ya kaya kama chakula na kugharamia mahitaji mengine ya msingi na wakati huo huo wakiboresha miundombinu katika jamii na kupata ujuzi na stadi za maisha.