Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

Wadau wa Maendeleo watembelea miradi ya TASAF


Mwakilishi wa Benki ya Dunia Wout Soer akizungumza wakati wa ziara ya Wadau wa Maendeleo mkoani Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani TASAF, Shedrack Mziray

Wadau wa Maendeleo wanatembelea miradi inayofadhiliwa na TASAF katika mikoa mitatu ya Mwanza, Mtwara na Arusha katika vijiji vilivyochaguliwa mikoani humo.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Mwanza, mwakilishi wa Benki ya Dunia Bw Wout Soer amesema inatia moyo kuona miradi ya TASAF inaendana na hali halisi ya maisha ya wananchi na kugusa maisha yao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani TASAF, Shedrack Mziray aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF amewashukuru wawakilishi wa Wadau wa Maendeleo kwa ufadhili wao na kuahidi ushirikiano mkubwa kutoka Serikalini na TASAF katika kuendeleza miradi hiyo kwa maslahi ya wananchi.

Amesena ziara ya Wadau hao ina lengo la kuangalia jinsi miradi inavyotekelezwa na itakuwa sehemu ya majadiliano na Serikali kuhusu kuongeza muda wa mradi kwa miaka miwili baada ya Septemba 2023.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Mkoa wa Mwanza, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana amewahakikishia wadau hao ushirikiano wa Serikali kuendeleza mradi na kuomba waendelee kufadhili miradi mingine ya maendeleo.

Wadau hao wanatembelea miradi inayotekelezwa wilayani Misungwi katika vijiji vya Maganzo, Mondo na Ng’wakalima Januari 12,2023 na Januari 13, 2023.

Sehemu ya washiriki wa kikao na Wadau wa Maendeleo jijini Mwanza