Habari
Kamati ya Taifa ya Uongozi yatembelea walengwa Wilayani Babati Mkoani Manyara

Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF wakiwasikiliza Walengwa wa Mpango walipokuwa wakitoa ushuhuda wa mafanikio yao katika Kijiji cha Minjingu Wilayani Babati.
Bi Elisifa el-Sangau akitoa ushuhuda mbele ya Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF jinsi alivyofanikiwa kwa kutumia ruzuku ya itolewayo na TASAF Kusomesha Watoto, Kuboresha Makazi, Kujiunga kwenye Kikundi cha Kuweka Akiba na Kukopa pamoja na kuanzisha biashara ya kusuka vikapu kutoka Kijiji cha Minjingu Wilayani Babati.
Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF wakiongozwa na kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw Charles Mwamaja kununua bidhaa zilizotengenezwa na walengwa kutoka Kijiji cha Minjingu Wilayani Babati
Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa wakimsikiliza Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF Bw Charles Mwamaj huku wakiendelea kusuka vikapu na mikeka katika Kijiji cha Minjingu Wilayani Babati
Bw Sifaeli Lengaramu akielezezaa mafanikio yake kwa kufuga kuku, mbuzi na ng’ombe mbele ya Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF Bw Charles Mwamaja, akimkabidhi fedha shilingi laki sita (600,000/-) Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Bi Anna Mbogo, zilizotolewa na wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF kwa ajili ya kukuza mitaji kwa vikundi sita vya walengwa wa TASAF vya kuweka Akiba na kukopa vya Kijiji cha Minjingu Wilayani Babati, kila kikundi kitapata shilingi laki moja.