Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

Kamati ya Uongozi TASAF yatembelea miradi Mbeya


Mratibu wa TASAF Mkoa wa Mbeya, Aika Temu akisoma Taarifa ya Mkoa mbele ya Kamati

USHAURI umetolewa kuwa miradi inayotelekelezwa na wanufika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa chini ya ajia za muda ikabidhiwe kwenye mamlaka nyingine za kiserikali kwa ajili ya kuwa endelevu.

Ushauri huo umetolewa Machi 30, 2022 na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Radhid Chuachua mbele ya Kamati ya Uongozi ya Kitaifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF iliyotembelea miradi ya mfuko huo mkoani humo.

Awali, Kamati ilipokea taarifa za miradi ya mfuko Mkoa wa Mbeya taarifa ya Wilaya ya Rungwe na ya kijiji cha Katumba wilayani humo na kutembela baadhi ya walengwa na miradi inayotekelezwa chini ya mpango wa ajira za muda

Dkt. Chuachua alisema ili kuhakikisha miradi hiyo inakuwa endelevu ni vema baada ya kukamilika ikakabidhiwa kwenye mamlaka husika za kiserikali ambazo zitaichukua na kuanza kuihudumua.

Akitoa mfano, alisema walengwa wanapotengeneza barabara ni vema zikakabidhiwa Mamlaka ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ambayo itazisajili na kuanza mpango wa kuziandisha viwango.

Dkt Chuachua alisema walengwa wanafanya kazi kubwa ya kuanzisha miradi ya maji na kutunza vyanzo vyakena itakuwa vema kama miradi hiyo itakuchukua na mamlaka za maji na hatimaye kuziingiza katika takwimu zake.

“Ingekuwa vema kama Mbeya UWSA (Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka Mbeya) katika tamwimu zake itasema mirdi kadhaa imetokana na TASAF na tukaona ni asilimia ngapi ya miradi ya maji iliyopo ili mchango huu mkuwa wa TASAF iweze kuingia katika rekodi,” alisema.

Awali, Mratibu wa TASAF Mkoa Mbeya, Aika Temu aliielezwa Kamati kuwa mkoa wake wenye jumla ya walengwa 51,767 katika vijiji 783 umepokea kiasi cha Sh 2.5 bilioni ambazo zimetumika katika kazi za ajira za muda zikijumuisha ujira, vifaa na usimamizi katika miradi ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali.

Aliitaja miradi hiyo kuwa ni utengenezaji wa mboni na kurutubisha ardhi, uhifadhi wa vyanzo vya maji, utengenezajiwa vivuko na miundombinu ya umwagiliaji.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Kitafa, Dkt. Naftari Ng’ondi aliupongeza uongozi wa Mkoa wa TASAF kwa ufuatiliaji mzuri na kushauri kujumuisha takwimu zake kuwa wa mkoa mzima badala ya kuonesha baadhi ya Maeneo ya Utekelezaji.

Naye Mjumbe wa Kamati hiyo, Richard Shilamba alishauri vikundi vya TASAF viunganishwe na wadau wengine wa kiserikali na wasio wa kiserikali wanaowea kutoa mikopo na misaada mbalimbali ili kuongeza nguvu katika kuwakwamua walengwa.

Katika kijiji cha Katumba, Kamati ilikutana na walengwa na kutembelea mradi wa utunzaji wa chanzo cha maji ulioibuliwa na walengwa na kuzungumza na wanufaika mbalimbali.

Mmoja walengwa, Atupele Mwasomola alisema amewea kusomesha watoto wake hadi elimu ya juu kutokana na kutumia vizuri ruzuku za TASAF na alikuwa anajenga nyumba ya kisasa ambapo alibakiza mabati matano kumalizia kuieleka.

 

Mmoja wa walengwa wa TASAF katika kijiji cha Katumba, Atupele Mwasomola akizungumza mbele ya  Kamati

Baada ya kumtembelea nyumbani kwake na kuona hali halisi, Wajumbe wa Kamati walimchangia kiasi cha Sh100,000 ili kumalizia kueeka nyumba yake.

Akiwa kijijini hapo, Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Dtk Vincent Aney aliwataka walengwa walioboresha maisha yao kufikiria ujitoa kwa hiari katika ruzuku ili kuwaachia rusfa hiyo wengine.

Akiifafanua, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga alisema Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa ni wa muda na elimu inatolewa ili wanaojikwamua waweze kujiondoa kwa hiari.