Habari
Katibu Mkuu Ikulu afanya ziara Ofisi za TASAF Dodoma

Katibu Mkuu Ikulu Ndugu Mululi Majula Mahendeka ametembelea Ofisi za TASAF Makao Makuu Dodoma siku ya Jumatatu tarehe 27 Februari, 2023 na kufanya kikao kazi na Kamati ya Uongozi ya TASAF, Timu ya Menejimenti pamoja na Watumishi wa TASAF.
Katika kikao hicho Katibu Mkuu Mahendeka alipongeza juhudi zinazofanywa na TASAF katika kupunguza umaskini kwa jamii ya Tanzania. Alieleza kuwa yupo tayari kushirikiana ili kuhakikisha kazi za TASAF zinakwenda vizuri ili kutimiza malengo ya Serikali. Aidha Katibu Mkuu Ikulu aliwakumbusha wajumbe wa kamati kusimamia vizuri utelekezaji na kuifikisha TASAF katika kiwango kizuri cha mafanikio ya utekelezaji na kuitaka Menejiment ya TASAF kufuata taratibu na miongozo yote ya uendeshaji ya Serikali na kufanya kazi kwa bidii, weledi na maarifa ili kuongeza ufanisi kwa kuzingatia sheria na taratibu za kazi.