the minutes and a sub-counter with the seconds. It is made of solid gold, but also their special styles bring a new echo to public and review modern ladies watches design. www.paneraireplica.co hublot replicas watches rolex deepsea replica The white lacquered dial in the upper right quarter of the watch features a blue minute track on the outside and printed roman numerals in black all around. replica iwcs breguet replica The Maurice Lacroix logo at 12 oclock is crisp and adds a finishing touch to the small dial. Just below the main dial is a small seconds indicator with another one of those bulky looking hands.

TASAF | Habari
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

Kaya 10,000 zanufaika na TASAF Wilayani Same


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Same, Annastazia Tutuba amesema kumekuwa na mafanikio makubwa katika utekelezaji wa miradi kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kuanzia mwaka 2015 wakati Mpango unaanza utekelezaji wilayani humo

Amesema miongoni mwa mafanikio hayo ni wananchi kuwa na kipato na hivyo kuweza kujikimu, kuanzisha miradi mbalimbali na kuwajengea uwezo wananchi wa namna ya kuibua miradi ya kujikwamua kiuchumi.

Wilaya ya Same ina kata 34 na vijiji 103 zenye kaya 10,000 zinazonufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. Mkurugenzi Tutuba alieleza pia kuwa katika utekelezaji wa TASAF makundi ya watu wote wenye uhitaji yamefikiwa na kupitia maboresho yaliyofanyika kumeongezwa ruzuku kwa ajili ya watu wenye ulemavu.

“TASAF imefanya jambo kubwa kuwagusa watu wenye ulemavu ili waweze kupata mahitaji ya msingi na fedha za kuanzisha miradi ya kujiongezea kipato,” alisema Tutuba.

Kupitia utekekezaji wa miradi mbali mbali, Mkurugenzi Tutuba amesema kwamba miradi na shughuli nyingine wanazofanya walengwa zimewajengea uwezo wa kuibua miradi, kuitekeleza na kupata ujuzi ambao wanautumia katika maisha yao ya kila siku

“Wamejiandaa vilivyo hata watakapoondolewa kwenye Mpango wamepata ujuzi wa kuibua miradi ya kujiendeleza kwa kutumia nguvu kazi iliyopo katika jamii yao,” alisema Tutuba.

Wilaya ya Same imeshapokea shilingi bilioni 4 ambazo zimelipwa kama ruzuku kwa walengwa 10,000. Walegwa hao wanaunganishwa katika vikundi vya kuweka akiba na kuwekeza ili kuwa na kipato endelevu.