Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

Mafunzo ya Kutumia Zana ya Tathmini Shirikishi Jamii


Mkurugenzi wa Mifumo, Ufuatiliaji na Mawasiliano Bw Fariji Mishael akifungua mafunzo ya Tathmini Shirikishi Jamii.

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF umetoa mafunzo kwa watendaji wake wa Mkoa wa Arusha ili kushirikisha jamii kufanya tathmini ya huduma zinazotolewa na uwajibukaji wa viongozi wa vijiji katika maeneo ya utekelezaji. Mafunzo hayo yaliyofanyika wilayani Meru,  Mkoani Arusha yalifunguliwa na Mkurugenzi wa Mifumo, Ufuatiliaji na Mawasiliano TASAF Bw Fariji Mishael.

 

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya tathmini shirikishi jamii wakifuatilia ufunguzi wa mafunzo hayo.

 

Afisa Ufuatiliaji wa TASAF Bw Majuto Kawambwa akitoa maelezo kuhusu zoezi la tathmini ya ushirikishwaji jamii kwa wajumbe wa Halmashauri ya Serikali ya Kijiji cha Kandashe, wilayani Meru, Mkoani Arusha.

 

Jengo la Watumishi wa Afya linalojengwa katika Kijiji cha Kandashe, wilayani Meru ambalo limefanyiwa tathmini katika zoezi la tathmini shirikishi jamii.

 

Washiriki wa mafunzo ya tathmini shirikishi jamii katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mifumo, Ufuatiliaji na Mawasiliano Bw Fariji Mishael.

 

 

Tanzania Census 2022