Habari
Maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi yanayofanyika katika Viwanja vya Ukumbi wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma 25/04/ 2022 hadi 1/5/2022
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania, Bw. Ladislaus Mwamanga (mwenye suti kulia) akiwa pamoja na watumishi wa TASAF na Wanufaika wa Mpango Kunusuru Kaya za Walengwa wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe Joyce Ndalichako akipata maelezo juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe Joyce Ndalichako, akisikiliza kwa makini faida za mazao ya bahari ya Mwani kutoka kwa Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa wa TASAF wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwan Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mnufaika wa Mpango alipotembelea banda la TASAF wakati wa Maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi

Mtaalam wa Mawasiliano wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, Bi. Zuhura Mdungi akimwelimisha mwananchi juu ya shughuli za Mpango wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi

Bi. Hadija Mchemba wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF akitoa maelezo kwa mwananchi aliyefika banda la TASAF wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi

Mnufaika wa Mpango wa TASAF kutoka Mlingotini, Bagamoyo Mkoani Pwani Bwana Machano Ali Jingalao akitoa maelezo ya bidhaa zake kwa mwananchi aliyefika banda la TASAF wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi

Watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania, pamoja na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa wa TASAF, baada ya kupokea cheti cha Ushiriki wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi
