Habari
Mhe. Ridhiwani Kikwete afanya ziara Itigi, Singida kushuhudia malipo kwa wanufaika

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akishuhudia hatua mbalimbali za malipo kwa Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa katika Kijiji cha Songambele Wilayani Itigi, Mkoani Singida
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete leo amefanya ziara katika Kijiji cha Songambele Wilayani Itigi, Mkoani Singida ili kushuhudia namna malipo kwa Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa yanafanyika.
Akiwa katika Kijiji cha Songambele, Mhes. Ridhiwani alipata fursa ya kuona hatua kwa hatua namna ambavyo Wanufaika hupokea ruzuku zao, Warsha za jamii na namna Wawezeshaji wanahudumia Walengwa na baadae kuongea na wananchi.
Aidha, aliwaasa wawezeshaji kuwalipa Walengwa fedha zao zote wanazostahili na siyo kidogo kidogo.
“Naomba Wanufaika wote wa TASAF nchini wapewe fedha zao zote zinazotakiwa na sio kuwapa kidogo kidogo kwa kuwa lengo ni kuwatoa katika dimbwi la umaskini linalowakabili” alisema Mhe. Ridhiwani.
Hapa ni picha mbalimbali za matukio katika ziara hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Kemilembe Lwota akimkaribisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Itigi
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Kemilembe Lwota (hayuko pichani) katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Itigi
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Kemilembe Lwota akitoa maelezo mafupi kwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Itigi
\Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akikaribishwa na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa katika Kijiji cha Songambele Wilayani Itigi, Mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa (hawako pichani) katika Kijiji cha Songambele Wilayani Itigi, Mkoani Singida.
Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa katika Kijiji cha Songambele Wilayani Itigi, Mkoani Singida wakimsiliza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayuko pichani).
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Viongozi mbalimbali waliofika kumpokea mara alipowasili katika Ofisi za Halmashauri ya Wilayani ya Itigi, Mkoani Singida.