Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

Mhe. Ridhiwani Kikwete Akagua Shughuli za Walengwa Mkoani Singida


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akiangalia mbuzi wanaofugwa na mmoja wa Walengwa kupitia ruzuku ya uzalishaji itolewayo na TASAF

Akiwa katika siku yake ya pili Mkoani Singida, Mhe. Ridhiwani Kikwete ametembelea na kukagua shughuli mbalimbali za Walengwa katika Manispaa ya Singida. Mhe. Ridhiwani Kikwete alipata bahati ya kutembelea katika Kijiji cha Ughaugha B, Halmashauri ya Manispaa ya Singida Mkoa wa Singida ambako pamoja na shughuli nyingine aliweza kuona mbuzi wa mmoja wa Walengwa kwa niaba ya wengine.

Yafuatayo ni baadhi ya matukio yaliyojiri katika ziara hiyo Mkoani Singida:

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Viongozi wakati akikaribishwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida Bi. Yagi Kiaratu (aliyesimama) akitoa taarifa fupi ya Halmashauri kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Manispaa ya Singida kwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete

 

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Bw. Stanslaus Choaji (aliyesimama) akimkaribisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani kuongea na Sekretarieti ya Mkoa wa Singida

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani akisaini kitabu cha wageni katika Kijiji cha Ughaugha B, ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Singida Mkoa wa Singida katika ziara yake ya kutembelea Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa

Baadhi ya Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani (hayuko pichani) katika Kijiji cha Ughaugha B, ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Singida Mkoa wa Singida