Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

Waziri Simbachawene aeleza waliyojifunza kuhusu Mradi Ajira za Muda Kwa Watu Wasiokuwa Na Uwezo


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti, Utumishi na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amesema ziara ya Mafunzo na kubadilishana uzoefu iliyofanyika nchini Afrika Kusini imesaida kuimarisha ushirikiano  katika kutekeleza shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa.

Waziri Simbachawene ameyasema hayo leo Machi 19, 2025 nchini Afrika Kusini wakati wa majumuisho ya ziara ya kimafunzo ya siku tano nchini humo kuhusu ajira za muda kwa watu wasiokuwa na uwezo, kama ambavyo nchini inavyotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF.

Waziri Simbachawene aliyeambatana na viongozi waandimizi wa TASAF, amesema nchi hiyo imepiga hatua katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo suala la ajira.

Pamoja na kuwawezesha na kuongeza Serikali ya nchi hiyo, haijaishia tu kuwezesha wasiokuwa ajira bali wanashughulika na ukosefu wa ajira.

“Mbali na kuwezesha watu wasiojiweza kupitia ajira wenzetu wamekwenda mbali zaidi kwa kutatua changamoto ya ajira kwa vijana waliosoma na wasiosoma, lakini pia wanawajenga ujuzi.

“Pia wenzetu wanashughulika na kuwaanda watu watakaoweza kufanya biashara, kimsingi ukosefu wa ajira na kupambana na umasikini haviachani.Wenzetu wametenga bajeti na wana wizara maalumu inayoshugulikia ajira za umma," amesema Waziri Simbachawene.

“Zaidi ya hayo vijana hao, wanajengewa uwezo na ujuzi wa kujitegemea na kuanzisha biashara zao au kwenda kujiunga na kuajiriwa na watu wengine.Pia wanajihusisha na kundi la watu masikini katika jamii kama ambavyo TASAF wanafanya,” amesema Waziri Simbachawene.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Shadrack Mziray amesema wamehitimisha ziara yao siku tano kwa kutembelea eneo la uhifadhi maalumu wa misitu lililopo nchini humo

“Pamoja na kufanya uhifadhi, eneo lina fursa ya ajira kwa walengwa ambao wapo mpango wa ajira za umma.Tulichojifunza katika hizi siku tulizokuwa hapa ni kwamba fursa zinapatikana siyo tu kwa kubuni vitu vipya bali tunaweza kushirikiana na Serikali au sekta binafsi kwa shughuli wanazozifanya zikawachukua walengwa wetu na kupata fursa za ajira,”amesema Mziray.