Habari
Mnufaika wa Ruzuku ya Uzalishaji Hamyawezi afanya makubwa ambayo wengine hawayawezi
Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa mkazi wa Mtaa wa Chuno katika Manispaa ya Mtwara Mikindani Bi. Hamyawezi Mshamu ambaye amepokea Ruzuku ya Uzalishaji amefanikiwa kuanzisha biashara ya kusuka ukili na kutengeneza mikeka. Biashara hiyo imemwezesha kuimarika kiuchumi na kujitegemea. Bi.Hamyawezi mwenye ulemavu wa miguu anafanya kazi kwa kujituma na imemsaidia kuendelea vizuri na biashara yake
Bi. Hamyawezi anawakilisha wanufaika wengi wa TASAF wenye moyo wa ujasiri katika kupambana na umaskini.