Habari
Kikao cha maandalizi ya Ziara ya Waziri wa Maendeleo wa Norway kutembelea miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

Mchumi wa Ubalozi wa Norway Bw. Olav Lundstol (aliyevaa jaketi ya kijivu) akijadiliana na maofisa wa TASAF (kulia) wakati wa kikao cha maandalizi ya ziara ya Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway kutembelea miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Waziri huyo, Mhe. Anne Beathe Tvinnereim na Balozi wa Norway nchini Tanzania watatembelea wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa katika Kijiji cha Chihembe, Kata ya Mvumi Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Jumatano Septemba 7, 2022
Maofisa wa Ubalozi wa Norway na maofisa wa TASAF walipomtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mhe. Dk. Semistatus H. Mashimba katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Septemba 1, 2022
Maofisa wa Ubalozi wa Norway, maofisa wa TASAF, maofisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na baadhi wa wanakijiji wakiwa katika picha ya pamoja katika Bwawa la Chaco kijjini Chihembe