Habari
Mziray ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Bwana Shedrack Salmin Mziray kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF kuanzia tarehe 03 Julai 2024.
Kabla ya uteuzi huu Bwana Mziray alikuwa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani (TASAF). Bwana Mziray alianza kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF terehe 01/07/2023 baada ya kustaafu kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji Bw. Ladislaus Joseph Mwamanga.