Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

TASAF yakamilisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya mfano kwa shilingi milioni 900


Wanafunzi wanaotoka katika kaya za Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa wakifurahia miundombinu ya shule ya Mfano ya Sekondari Igogwe katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoa wa Mwanza iliyojengwa na TASAF kwa gharama ya shilingi milioni 900

Ujenzi wa nyumba za walimu katika shule ya mfano ya Sekondari ya Igogwe Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mkoa wa Mwanza upo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji wake. Hii ni sehemu ya utekelezaji wa miradi ya uendelezaji wa miundombinu unaofanywa na TASAF

Muonekano wa baadhi ya matanki na miundombinu ya maji iliyowekwa katika shule ya mfano ya Sekondari ya Igogwe iliyojengwa na TASAF katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mkoa wa Mwanza

Ujenzi wa shule ya mfano ya Sekondari ya Igogwe Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mkoa wa Mwanza ikiwa ni miongoni mwa miradi iliyotekelezwa na TASAF umehusisha vyoo na bafu za kisasa katika mabweni ya wanafunzi pamoja na vyoo vya walimu

Wanafunzi wa shule ya mfano ya Sekondari ya Igogwe Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela iliyojengwa na TASAF wakiwa katika maabara ya Fizikia

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF umekamilisha ujenzi wa shule ya Mfano ya Sekondari ya Igogwe katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mkoa wa Mwanza kwa gharama ya shilingi milioni 900.

Shule hiyo ina majengo mbalimbali ikiwemo jengo la utawala, vyoo, maktaba ya kisasa yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 54 pamoja na maabara za kisasa kwa ajili ya masomo ya Fizikia na Kemia ambazo zina samani na vifaa vyote vya kujifunzia.

Pia TASAF imejenga mabweni mawili ambapo moja la wasichana lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 limekalimika wakati bweni lingine na nyumba ya walimu vipo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji wake.

Miongoni mwa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo ni pamoja na wanaotoka katika kaya za walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF.

Katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma zote muhimu shuleni hapo, TASAF imeweka miundombinu ya maji kwa  kutumia tenki  zenye ujazo wa lita 40,000 sambamba na kufunga mfumo wa umeme wa Jua  (Solar) wakati Serikali ikiwa katika