Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

Mkutano wa Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango wa TASAF Kipindi cha Pili


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Shedrack Mziray akiwa na Kiongozi wa Shughuli za TASAF nchini Tanzania Bi. Claudia Taibo kutoka Benki ya Dunia pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Bw. Salhina Mwita Ameir wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango wa TASAF Kipindi cha Pili uliofanyika katika ukumbi wa mikutano jijini Dar es Salaam

Viongozi wa Serikali, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF pamoja na Wadau wa Maendeleo wameanza mkutano wa mapitio ya pamoja ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa pamoja na ziara ukaguzi wa kila baada ya miezi sita wa kazi za TASAF.

Mapema jumatatu Januari 29, 2024, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Shedrack Mziray aliongoza mkutano wa majadiliano uliowaleta pamoja Uongozi wa TASAF, wawakilishi wa Serikali, na Washirika wa Maendeleo. Bi. Claudia Taibo Zambra ambaye ni Kiongozi wa Shughuli za TASAF kutoka Benki ya Dunia, alikuwepo pia wakati wa tukio hilo.

Sehemu ya washiriki wakifuatilia hoja mbalimbali zikiwasilishwa

Baada ya mkutano huo, TASAF, wawakilishi wa Serikali, na Washirika wa Maendeleo walifanya ziara za ukaguzi katika Mamlaka nne za utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa ambayo ni Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba pamoja na Halmashauri za wilaya  za Rungwe, Mufindi na Moshi.

Katika Mamlaka ya Utekelezaji ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, timu ililenga kutathmini miradi ya kuboresha kipato, Ajira za Muda, Malipo ya Kielektroniki, na Uhifadhi wa Mazingira. Aidha, katika malmaka ya utekelezaji Rungwe, timu ililenga kujionea miradi kama hiyo.

Katika Mkoa wa Kagera Manispaa ya Bukoba, lengo lilikuwa kwenye Malipo ya Kielektroniki na Ulinzi, Timu nyingine itakuwa Mufindi DC, ikizingatia Miradi ya Ajira za Muda , Miradi ya kuboresha Kipato pamoja na  Uhifadhi wa Mazingira.

Ziara hiyo inatarajiwa kumalizika Februari 9, 2024, na majadiliano juu ya maeneo maalum na kuweka maazimio.