Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

TASAF katika Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha


Mfuko wa Maendeleo ya Jamii ni miongoni mwa washiriki wa maonyesho ya wiki ya huduma za fedha yanayoendelea katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha. Maonyesho hayo yameanza rasmi Jumatatu Novemba 20 na yatazinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Katika maonesho hayo, walengwa wa TASAF wanaonesha bidhaa wanazotengeneza na kuuza zikiwemo sabuni, ufugaji wa kuku, mikeka, vikapu na bidhaa za urembo. Walengwa hao watapata fursa ya kuhudhuria semina zinazotolewa kila siku kuhusu huduma za fedha na namna wanavyoweza kuzitumia ili kukuza pato la mtu mmoja mmoja.