Habari
TASAF yashiriki Maonesho ya Nane Nane kitaifa jijini Mbeya

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, unashiriki Maonesho ya Kilimo Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Katika maonesho hayo, wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa wanaonesha shughuli mbalimbali za kiuchumi wanazozifanya kwa lengo la kujiingizia kipato cha kaya zao.
Miongoni mwa shughuli zinazofanywa na walengwa wanaoshiriki maonesho haya ni pamoja na ufugaji wa kuku, kushona mikeka, utengenezaji wa sabuni kwa ajili ya matumizi mbalimbali, viungo mbalimbali vya vyakula, ufumaji wa masweta pamoja na kutengeneza batiki.
Ndani ya viwanja ya John Mwakangale, banda la TASAF linapatikana katika barabara ya Ibunge. TASAF pia inajenga uelewa wa shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Mfuko.
Maonesho haya yalifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Philip Mpango siku ya Jumanne Tarehe 1 mwezi wa nane mwaka huu.
Maonesho ya kilimo ya waka huu yanafanyika chini ya kauli mbiu ya kitaifa ‘Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula’.
Mgeni aliyetembelea banda la TASAF akipata maelezo kuhusu Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa