Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

TASAF, Mtakwimu zakubaliana kutatufa taarifa Zanzibar


Mfuko wa Maendeleo ya Jamii  - TASAF umeingia makubaliano na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar kwa ajili ya kukusanya taarifa za zitakazowezesha kutathimini kiwango cha kuondoa umasikini.

 

Makubaliano hayo yalitiwa saini Julai 23, 2021 katika Ofisi za TASAF jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo, Ladislaus Mwamanga na Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Zanzibar Mayasa Mahfoudh Mwinyi.

 

Akizungumza kabla ya utiaji saini huo, Mwamanga alisema kazi ya kuondoa umasikini inayofanywa na Serikali kupitia TASAF inapaswa kupimwa ili kujua kwa kiwango gani umasikini umeondolewa.

 

Naye Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar, Mayasa alisema ana imani na matokeo chanya ya kazi inayofanywa na TASAF Zanzibar na kwamba takwimu zitakazokusanywa zitaweza kusaidia utafiti wa kupima kiwango cha umasikini kilichoondolewa.

 

Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar itakusanya taarifa hizo kwa upande wa Tanzania Zanzibar wakati Tanzania Bara kazi hiyo itafanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) chini ya makubaliano tofauti.