Habari
TASAF yakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kinyikani Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba

TASAF yakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kinyikani Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Visiwani Zanzibar kilichozinduliwa tarehe 3/1/2025 na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid ikiwa ni sehemu ya Shamrashamra za Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kituo hiki kilichojengwa sambamba na nyumba ya watumishi, kinalenga kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wakazi wa Kojani na Wilaya ya Wete ambao hapo awali hawakuwa na kituo cha afya.