Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

TASAF yashiriki Maonesho ya NANENANE 2023


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango akifungua Maonesho ya Wakulima Maarufu kama NANENANE Yanayofanyika katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya

Mfuko wa Maendeleo ya jamii TASAF unashiriki katika maonesho ya sikukuu ya wakulima maarifu kama nane nane yanayofanyika Jijini Mbeya katika Viwanja vya John Mwakangale. Maonesho hayo yatakayofanyika kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti 2023, yamefunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango

TASAF inashiriki maonesho hayo ikiwa imeambatana na  walengwa 12 wa Mpango wa Kunusuru kaya za walengwa ambao wanaonesha na kuuza bidhaa mbali mbali ambazo zinatokana na miradi wanayotekeleza ikiwemo mikeka, nguo, maziwa, mikate na mazao

Baadhi ya Walengwa wa TASAF wakiwa kwenye Maonesho ya Wakulima NANENANE yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya