Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

Dkt. Mpango ataka changamoto TASAF zishughulikiwe


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ametaka changamoto mbalimbali katika Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF zishughulikiwe ili mfuko huo uendelee kufanya kazi kwa ufanisi.

Amesema hayo Alhamisi Novemba 24, 2022 alipotembelea banda la TASAF katika Maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha yanayoendelea jijini Mwanza.

Dkt. Mpango amesema wapo walengwa ambao wanapata shida kufikiwa na huduma za TASAF za malipo kwa njia ya kielektroniki kutokana na kukosa vitambulisho vya NIDA na wengine wanaostahili kupata ruzuku za TASAF wanaondolewa kwenye Mpango kutokana na kutokuwa na taarifa sahihi kutoka maeneo yao.

Amesema kuwa ni jukumu la watendaji wa TASAF kuwa wabunifu kushughulikia matatizo ikiwemo kukosekama kwa vitambulisho kwa kuwa hata Serikali haijaweza bado kuwapatia wananchi wote vitambulisho vya Taifa.

Mhe, Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala w TASAF Bw Godwin Mkisi alipotembelea banda la Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF

 

Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiongea na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa alipotembelea banda la Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF