Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

TASAF yazindua Taarifa ya Utafiti wa Mafanikio ya Mpango


Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF umezindua taarifa ya utafiti wa mafanikio ya awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa

Uzinduzi huo umefanyika Ijumaa Julai 15, 2022 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mwakilishi kutoka Benki ya Dunia na wadau wengine wa maendeleo.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa katika ukumbi wa mikutano wa TASAF – Dar es Salaam.

 

Utafiti huo uliofanywa kwa ushirikiano na Ofisi ya Taifa ya  Takwimu – NBS na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar – OCGS ulikamilika mwaka 2019 lakini haukuweza kuzunduliwa kutokana na changamoto ya ugonjwa wa UVIKO-19, lakini, hata hivyo taarifa zake zimekuwa zikitumika .

Utafiti huo ulioonesha mafanikio ya Mpango umefanyika katika Maeneo ya Mamlaka ya Utekelezaji – PAA 18, mbili kutoka Tanzania Zanzibar na 16 kutoka Tanzania Bara.

 

Kiongozi wa Shughuli za TASAF kutoka Benki ya Dunia Michelle Zini akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa katika ukumbi wa mikutano Ofisi za TASAF – Dar es Salaam.

 

Katika maeneo hayo, jamii 330 zilichaguliwa, 240 kutoka Tanzania Bara na 90 kutoka Tanzania Zanzibar na kuwekwa katika makundi matatu moja linalopata ruzuku ya masharti, jingine linalopata ruzuku ya masharti, ajira za muda na akiba na ukuzaji wa uchumi wa kaya huku kundi jingine likitumika kama rejea ya utafiti

 

Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa katika ukumbi wa mikutano TASAF Dar es Salaam.

 

Kwa mujibu wa utafitu huo, matumizi ya huduma za jamii kama zile elimu na afya yameongezeka katika kipindi cha Mpango huku udahili wa wanafunzi katika Shule za Msingi nao ukipanda kutokana na utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa.

Idadi ya walengwa wenye Bima ya Afya nayo imeongezeka mara tatu huku umiliki wa rasilimali zalishi ukipanga kwa 18.6%

Kiongozi wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia Michelle Zini alisema Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa ni moja ya mipango bora na yenye tija duniani inayogusa wadau moja kwa moja.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF aliwashukuru wadau wa maendeleo pamoja na NBS na OCGS kwa utafiti huo ambao utakuwa dira katika kuendelea na utekelezaji wa Mpango