Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

Uzinduzi wa Kamati ya Taifa ya Uongozi TASAF


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama, amezindua Kamati ya Uongozi ya TASAF Jumamosi 24 Septemba 2022. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano, TASAF Dodoma.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi za TASAF Makao Makuu Dodoma.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akikabidhi cheti kwa Katibu Mkuu Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi TASAF iliyomaliza muda wake. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga

 

 

Mwenyekiti Mpya wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF Bw. Peter A. Ilomo akiongea wakati wa Uzinduzi wa Kamati hiyo

 

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF (waliokaa mstari wa mbele) wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Uongozi ya TASAF Taifa

 

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF na Katibu wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF akiwakaribisha wageni waalikwa katika Hafla ya Uzinduzi wa Kamati ya Uongozi TASAF Taifa

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi baada ya uzinduzi wa Kamati ya Uongozi TASAF Taifa. Kutoka kushoto ni Kiongozi wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia, Michele Zini, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi TASAF Taifa Bwana Peter Ilomo, Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka 

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (katikati ya waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF. baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa TASAF wakiwa Makao Makuu ya TASAF Dodoma.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (katikati - waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF.