Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

Wadau wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) Wakutana Kutathmini Mifumo ya Malipo ya Walengwa na Kujadili Changamoto zinazojitokeza


Wadau mbalimbali wa Mpango wa TASAF wamekutana jijini Arusha katika mwendelezo wa vikao kazi kutathmini utekelezaji wa miongozo ya malipo, kujadili na kutafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazojitokeza wakati wa malipo.

Kikao kazi,  ambacho kimefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Kibo tarehe 24.03.2024, kimewakutanisha wadau hao pamoja na Menejimenti ya TASAF ili kwa pamoja kuweza kutathmini mafanikio na kubaini changamoto zinazojitokeza wakati wa dirisha la malipo na kuzitafutia ufumbuzi ili kuboresha ufikishaji wa fedha za walengwa na kupunguza malalamiko.

Wadau walioshiriki ni Benki za NMB, CRDB na PBZ, Mitandao ya Vodacom, Airtel na Tigo, pamoja na Wizara ya Fedha (GePG), NIDA na TAMISEMI

Habari picha ni kama inavyoonekana hapa chini:

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Shedrack Mziray (aliyesimama) akiongea na Wadau wa Malipo ya Walengwa wa TASAF kwa Njia ya Kielektroniki katika Mkutano uliofanyika tarehe 25.03.2024 katika Ukumbi wa Hoteli ya Kibo jijini Arusha

Meneja wa Uhawilishaji Fedha kwa Walengwa wa TASAF Bw. Seleman Masala (aliyeshika kipaza sauti) akielezea jambo wakati wa Mkutano wa Wadau wa Malipo ya Walengwa wa TASAF kwa Njia ya Kielektroniki uliofanyika tarehe 25.03.2024 katika Ukumbi wa Hoteli ya Kibo jijini Arusha

Mratibu wa Malipo kwa Njia ya Kielektroniki wa TASAF, Bi. Josephine Joseph (mwenye kipaza sauti) akieleza jambo wakati wa Mkutano wa Wadau wa Malipo ya Walengwa wa TASAF kwa Njia ya Kielektroniki uliofanyika tarehe 25.03.2024 katika Ukumbi wa Hoteli ya Kibo jijini Arusha

Baadhi ya Wadau wa Malipo ya Walengwa wa TASAF kwa Njia ya Kielektroniki wakishiriki Mkutano wa Wadau hao uliofanyika tarehe 25.03.2024 katika Ukumbi wa Hoteli ya Kibo jijini Arusha

Wakishiriki wa Mkutano wa Wadau wa Malipo ya Walengwa wa TASAF kwa Njia ya Kielektroniki wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufunga Mkutano wao uliofanyika tarehe 25.03.2024 katika Ukumbi wa Hoteli ya Kibo jijini Arusha