the minutes and a sub-counter with the seconds. It is made of solid gold, but also their special styles bring a new echo to public and review modern ladies watches design. www.paneraireplica.co hublot replicas watches rolex deepsea replica The white lacquered dial in the upper right quarter of the watch features a blue minute track on the outside and printed roman numerals in black all around. replica iwcs breguet replica The Maurice Lacroix logo at 12 oclock is crisp and adds a finishing touch to the small dial. Just below the main dial is a small seconds indicator with another one of those bulky looking hands.

TASAF | Habari
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

Wafanyakazi TASAF watakiwa kuzingatia maadili


Wafanyakazi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF wametakiwa kufanya kazi kwa ueledi na kuzingatia maadili huku wakiepuka ubaguzi wa aina yoyote katika utekeleaji wa majukumu yao.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi Aprili 27, 2023 na Katibu Mkuu Ikulu, Mululi Mahendeka alipokuwa akifungua Mkutano wa Mwaka wa wafanyakazi hao unaofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa APC Bunju, Dar es Salaam,

Bw Mahendeka amesema kwa moja ya changamoto zinazoukabili mfuko huo ni baadhi ya wanasiasa kupotosha lengo halisi ya Mfuko na kuhusisha kazi zake na itikadi za kisiasa na ukabila.

Amesema kwa kuwa wako wanasiasa, kwa malengo wanayoyajua wao, wamekuwa wakieneza habari potofu kuwa kazi wa Mfuko zinahusiana na ikitadi za kisiasa, ni jukumu la wafanyakazi kurekebisha dhana hiyo kwa kutoa habari ili wananchi waelewe kwa mba TASAF haina ubaguzi wa itikadi za kisiasa, kidini na kikabila bali ipo kwa ajili ya kusaidia wananchi maskini wanaoishi katika mazingira magumu.

ASAF ni taasisi ya Serikali na hivyo inafuata taratibu za kiserikali. Hakikisheni mnafanya kazi kwa bidii ueledi na maarifa. Fuateni miongozo ya Serikali ikiwemo kutunza siri za Serikali,” amesema.

Ameitaka Menejimenti ya TASAF kutambua majukumu yake na kuyatekeleza kwa ukamilifu , kutembelea miradi katika mamlaka za utekelezaji, kuzungumza na walengwa na kujua changamoto zao ii iwe rahisi kuzitatua. “Fanyeni kazi sawasawa na jina la Mfuko na muweke kipaumbele kwa maendeleo ya jamii,” ameasa.

Aidha amewataka wafanyakazi kutunza rasilimali za taasisi ikiwemo magari, kompyuta. mifumo na kompyuta mpakato na kufanya kazi zilizopo na kulingana na sera kukidhi matarajio ya Serikali kwa mfuko huo

“Mambo ya uendeshaji wa miradi yameainishwa vizuri katika andiko la mradi lililosainiwa kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo. Someni andiko la mradi kwa makini ili mjue mnachotarajiwa kufanya,” amesema.

Akitoa shukurani kwa Katibu Mkuu Ikulu kwa nasaha zake, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Kitaifa ya TASAF, Peter Ilomo amesema Kamati yake na Menejimenti itazingatia maelekezo hayo.