Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

Wanufaika wa TASAF Igagala Wako Tayari Kuhitimu


Wanufaika wa TASAF wa Kijiji cha Igagala Wilayani Wanging'ombe wamekiri kuwa tayari kutoka kwenye Mpango wa TASAF kwa kuwa imewafikisha mahali pazuri kiuchumi.

Baadhi ya wanufaika waliohudhuria warsha ya jamii ambayo inafanyika kabla ya malipo, walionyesha utayari wa kutoka kwenye Mpango na kusitishiwa ruzuku na kukiri kwamba TASAF imekuwa msaada sana kwenye maisha yao. 

“Mimi nina dada zangu wawili ambao ni walemavu. Nimepata nafuu katika kuwahudumia kupitia TASAF na nimewajengea nyumba yao, wana shamba la parachichi la robo tatu eka, wanafuga nguruwe na kusomesha watoto wao. Kweli TASAF ni mkombozi wa wanyonge” aliongea Bw. Efrahim Jacob Mgaya wa Kitongoji cha Njiapanda kijijini Igagala ambaye ni mmoja wa wanufaika aliye tayari kutolewa kwenye Mpango na kuwapisha wengine wenye uhitaji kuingia.

Aidha, Mtendaji wa Kijiji cha Igagala Bi. Sharifa Kunga alisema TASAF imeacha alama kubwa katika kijiji cha Igagala kwani maisha kwa ujumla ni mazuri kwa sababu uchumi wa wananchi umekua, parachichi zinapandwa kwa wingi, ufugaji umeongezeka, nyumba bora na za kisasa zimeongeza na hivyo kijiji kuongezeka hadhi yake kiwilaya.

Mbali na kuhudumia walengwa, TASAF kwa kushirikiana na wanachi wa Igalala imejenga imejenga mawili, ofisi ya walimu moja na matundu sita ya vyoo, Aidha katika madarasa hayo kumewekwa madawati 52 na makabati mawili. Moja ya madarasa hayo yanatumiwa na wanafunzi wa darasa la Pili wa shule hiyo. Wakati huo huo mchakato wa ujenzi wa zahanati ya Igagala kupitia TASAF unaendelea.

Wanafunzi wa darasa la pili wa shule ya msingi Igalala wakiwa darasani. Shule hiyo iko katika kijiji cha Igagala, Kata ya Ulembwe Wilayani Wanging’ombe