Habari
Wanufaika wa TASAF Zanzibar wajikwamua kiuchumi

Wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wameushukuru Mfuko huo kwa kuwawezesha na kuwasaidia kuinua vipato vyao na familia zao kwa ujumla. Wametoa pongezi hizo mbele ya Wadau wa Maendeleo walipotembelea baadhi ya wanufaika katika Shehia ya Chumbuni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Wakizungumza kuhusiana na mafanikio yao, baadhi ya wanufaika hao wamesema awali walikuwa wakiishi maisha ya kubangaiza lakini baada ya kuja Mpango huo wa kunusuru kaya za walengwa wameinuka na kwasasa maisha yao yanaendelea kuneemeka. Kupitia kipengele hicho walengwa wamepatiwa fursa za kuunda vikundi na kupatiwa mafunzo ya stadi za maisha, vikundi hivyo vinaendelea na shughuli za uzalishaji zikiwemo ufugaji, kilimo cha mbogamboga na baishara ndogondogo.
Mmoja wa Wanufaika wa Mpango akitoa ushuhuda ya namna alivyojikwamua kiuchumi katika Shehia ya Chumbuni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja
Mchunga Ali Mbigili amesema wakati anaingia kwenye Mpango huo alikuwa akipata Sh36,000 lakini kadri siku zilivyokuwa zinaendelea akawa maisha yake yanazidi kuimarika.
Mwanamke huyo anayejishughulisha na ujasiriamali wa kushona nguo na mikoba, amesema alipata ruzuku ya Sh500,000 kisha akaazisha biashara hiyo na kwa siku anapata faida ya Sh20,000 ambayo anajiwekeza kwenye vikundi na kuweka akiba.
Mnufaika wa Mpango Bi. Mchunga Ali Mbigili akionesha mkoba aliotengeneza katika Shehia ya Chumbuni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja
“Nimesomesha watoto wangu kwenye fedha hii, nasuka vikapu na kushona nguo, kwakweli nimehitimu kutroka kwenye Mpango ila nashukuru tumepata faida kubwa na maisha yetu yameinuka
Mwingine, Keji Ali Juma, yeye amesema aliingia kwenye Mpango akiwa anapata Sh61,000 lakini kwasasa amehitimu akiwa na mashine ya kuhoka mikate na keki ambayo amekuwa maarufu kwa ajili ya kuwatengenezea wananchi katika shehia hiyo.
“Mpango huu umenisaidia sana, kutoka kwenye kula mlo mmoja hadi kula milo mitatu, tunaomba uendelee kuwasidia wengine amabo wanauhitaji nao waweze kusaidika katika maisha yao,” amesema
Mnufaika wa Mpango Bi. Keji Ali Juma akionesha bidhaa zake alizotengeneza katika Shehia ya Chumbuni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Shadrack Mziray amesema kwa kawaida wamekuwa na mapitio ya utekelezaji kila baada ya miezi sita hivyo wapo kwenye mapitio ya kawaida.“Amesema wanaelekea katika kipindi cha mwisho kinachoishia Septemba mwaka huu, amesema.
“Kikubwa tulichoona leo ni mafanikio makubwa ambayo yamepatikana kuzinyanyua kaya masikini, wengi wao waliotoka kwenye Mpango ni wale ambao wamepewa ruzuku ya kila baada ya miezi mwili waliongezewa ya kuendeleza miradi yao ambayo ni wastani wa Sh350,000,” amesema.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Shedrack Mziray
Amesema pamoja na programu hiyo licha ya kwenda ukingoni katika awamu ya pili, lakini wamekubaliana kwamba kuwe na programu nyingine ambayo ikianza kutekelezwa itachukua wale ambao hawakuwa kwenye program zilizioisha na inatarajia kuaza Septemba au Oktoba mwaka huu.
Kiongozi wa Shughuli za TASAF nchini Tanzania Bi. Claudia Taibo
Nao Wadau hao wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia na Ubalozi wa Ireland wameeleza jinsi walivyoridhishwa na Mpango huo unavyotekelezwa baada ya kushuhudia simulizi mbalimbali za wanufaika hao.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Salhina Mwita Ameir amesema wananchi wanafarijika kwa miradi hiyo kama yalivyo malengo ya TASAF yenyewe.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Bw. Salhina Mwita
“Kupunguza umaskini kuna njia nyingi, kuna kupunguza umaskini kupitia sekta ya elimu, afya na fedha kwa kupata kipato pamoja na masuala ya kimazingira yote lengo lake ni kuwaweka katika mazingira mazuri,” amesema.