Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amepongeza TASAF kwa kuwawezesha wanufaika wa Mpango


Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa amepongeza Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), kwa kuwawezesha wanufaika wa mfuko huo ikiwemo kuwasimamia katika shughuli za kiuchumi wanazofanya.

Waziri Majaliwa ametoa pongezi hizo leo jijini Arusha,alipotembelea banda la TASAF katika maonyesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha yanayifanyika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid.

"Niwapongeze TASAF mnafanya vizuri na tumeshuhudia matunda yenu nitatoa ujumbe kwa Wakurugenzi wa Halmashauri,waendelee kuwasaidia na  wawatengenezee maonyesho katika ngazi ya mikoa na wilaya,"alisema

"Nitatoa maelekezo wanufaika walioanza ujasiriamali wasaidiwe kupata masoko.Nitaagiza wakurugenzi watambue na wawatafutia masoko wajasiriamali,hata ukiamua kufuga kuku au mbuzi masoko yako na hoteli zipo,msiwe na shaka,"

Kaimu Mkurugenzi wa TASAF,Shedrack Mziray,alisema hadi sasa wameweza vikundi zaidi ya 56,000 vyenye wanachama 7,060 ambao wamejiongeza na kufanya ujasiriamali.

Mmoja wa wajasiriamali kutoka kikundi cha Naisula Kata ya Olasiti,Arusha,Tatu Hongoa alisema bado wanakabiliwa na changamoto ya masoko na mitaji yao bado siyo mikubwa.

"Tuna changamoto ya masoko ya bidhaa zetu na niwoambe wananchi wenzangu waliinufaika na TASAF wawe waangalifu kwani ukisaidiwa leo kuna ukomo wa msaada lazima uwe mwangalifu ujisaidie na wewe,"alisema