Habari
Waziri Simbachawene azungumza na wakazi wa Migoli kuhusu TASAF

Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (MB) akizungumza na wakazi wa kijiji cha Migoli Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa unaotekelezwa na TASAF
Wakazi wa Kijiji cha Migoli Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakimsikiliza Mhe. Waziri Simbachawene kwenye mkutano maalum wa kuzungumza na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa unaotekelezwa na TASAF
Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (MB) akisikiliza maoni ya wanufaika wa Mpango wa TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Veronica Kessy akitoa salamu za ukaribisho na kuufungua mkutano maalum wa Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa uliofanyika kwenye Kijiji cha Migoli
Katibu Tawala Msaidizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Ndg. Venance Petro Ntyalundura akitoa taarifa ya maendeleo ya miradi inayotekelezwa na TASAF kwenye mkutano wa Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa uliofanyika kwenye Kijiji cha Migoli