Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

Waziri Simbachawene azuru kituo cha afya Nyabilezi Chato


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora George Simbachawene ametembelea kituo cha afya Nyabilezi wilayani Chato akiwa katika ziara Mkoani Geita.

Kituo hicho kilichojengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh1.4 bilioni kinahudumia zaidi ya wananchi 19,000 wa kata ya Bukome na kata za jirani.

Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho Waziri Simbachawene amesema ili kuwajengea watu uwezo kiuchumi, Serikali imepeleka shilingi Bilioni 8.7 Wilayani Chato ili kupitia TASAF ili kutekeleza miradi. 

Baadhi ya wanufaika wa TASAF wamesema mpango huo umewabadili maisha na sasa wanaweza kupata chakula cha uhakika, kuanzisha ufugaji wa kuku na mbuzi unaowawezesha kupata kipato na kujikwamua kiuchumi.

Mmoja wa wanufaika hao Baraka Mugisha mkazi wa Nyabilezi amesema kupitia mpango wa TASAF ameezeka nyumba yake kwa bati baada ya kufanya kazi kwenye miradi ya ajira za muda kwa walengwa.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Chato Merdad Kalemani ameishukuru Serikali kupeleka miradi kwenye Wilaya hiyo ambayo mbali na kuwasaidia wananchi kupata kipato pia imewezesha miradi mbalimbali ya kiuchumi ukiwemo ujenzi wa vituo vya afya na miundo mbinu ya barabara na elimu