Habari
Ziara ya Mhe. Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Elisabeth Jacobsen na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la NORAD Bw. Bard Vegar Solhjell katika Kijiji cha Vikuge, Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani

Mapokezi ya Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bi. Elisabeth Jacobsen na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Norad Bw. Bård Vegar Solhjell pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga, walipowasili kijijini Vikuge
Mhe. Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bi. Elisabeth Jacobsen na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Norad Bw. Bård Vegar Solhjell pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga, wakisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Vikuge
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Norad Bw. Bård Vegar Solhjell akiwasilimu na kutoa shukrani zake za mapokezi mazuri kwa wanakijiji wa Vikuge
Mhe. Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bi. Elisabeth Jacobsen akiwasalimu wanakijiji cha Vikuge
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga, akiwapa maelezo wageni kutoka ubalozi wa Norway kabla ya kwenda kutembelea bwawa la kuhifadhia maji katika Kijiji cha Vikuge
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (aliyevaa suti ya kaki) akimpa maelezo jinsi bwawa la kuhidhia maji katika kijiji cha Vikuge lilivyojengwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Norad Bw. Bård Vegar Solhjell (aliyeshika miwani)
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Norad Bw. Bård Vegar Solhjell, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Bi Butamo Ndalahwa (mwenye shati jekundu) Mhe. Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bi. Elisabeth Jacobsen na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga, pamoja na watumishi wa Halmashari ya Kijiji, Halmashauri ya Wilaya na TASAF Makao Makuu.