Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

Ziara ya Wadau wa Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Bw. Shauri Selenda, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa kwa wadau wa maendeleo walipomtembelea ofisini kwake (hawapo pichani)

Meneja wa Programu ya Maendeleo jumuishi ya kiuchumi kutoka ubalozi wa Sweden Bi. Annie Sturinge akiuliza swali wakati wa ziara ya wadau wa maendeleo na maafisa wa TASAF baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa.

Mkurugenzi wa Progamu za Jamii Bw. John Elisha(wa tatu kulia) akiwa na Wadau wa Maendeleo wakati wa mazungumzo na kikundi cha kuweka na kuwekeza Tupendane (hawapo pichani) katika kijiji cha Kaole, wilayani Bagamoyo

Kikundi cha kuweka na kuwekeza Tupendane wakionyesha bidhaa zilozotengenezwa wakati wa ziara na wadau wa maendeleo kutoka ubalozi wa Sweden na Ireland.

Afisa Programu, Maendeleo katika ubalozi wa Irish (kulia) akiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na kikundi cha kuweka na kuwekeza Tupendane wakati wa ziara ya wadau wa maendeleo katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kijiji cha Kaole.

Meneja wa kuweka akiba na kukuza uchumi wa kaya Bi. Saraha Mshiu akipata maelezo kutoka kwa katibu wa kikundi cha Tupendane Bi. Tatu Mwinyi alipomtembelea kwenye mgahawa wake wakati wa ziara ya wadau wa maendeleo katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kijiji cha Kaole.

Bi. Tatu Mwinyi kutoka kikundi cha Tupendane akiwa amesimama mbele ya mgahawa wake aliouanzisha baada ya kupokea ruzuku ya uzalishaji mali

Bi.Furaha Juma kutoka kikundi cha Tupendane akionyesha biashara yake ya samaki wakati ya ziara ya wadau wa maendeleo katika kijiji cha Kaole, Bagamoyo

Wadau wa Maendeleo wakipata maelezo kutoka kwa Bi.Furaha Juma jinsi alivyojikwamua kiuchumi baada ya kupokea ruzuku ya uzalishaji mali katika kijiji cha Kaole, Bagamoyo