Habari
Sauti ya Mabadiliko: Stawisha Maisha inavyostawisha maisha kupitia redio Tanzania

Katika kijiji cha pembezoni, kando ya Ziwa Nyasa Kusini mwa Tanzania, redio ndogo inakuwa kitovu cha wanajmii kukutana. Wakati muziki wautambulisho wa kipingi cha Stawisha Maisha inapigwa, watu wanaacha shughuli zao za kawaida na kuwahi mahali pa kukutania kusikiliza kwa kipindi. Hii si burudani tu ni jukwaa lenye nguvu la kuwawezesha watu na kuleta mabadiliko katika jamii.
Stawisha Maisha ni mfululizo wa vipindi vya redio vinavyoandaliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa msaada kushirikiana na UNICEF. Lengo ni kujenga uelewa wa wanufaika wa TASAF kuhusu masuala ya kinga ya jamii,mintarafu masuala ya lishe hasa kwa Watoto wenye umri usiozidi miaka mitano na akina mama wajawazito.
Kikitangaza kwa Kiswahili katika mikoa 23, kipindi hiki kinawafikia watu wengi, wanaokisilikiza katikam maeneo ya wazi na kwenye mikutano ya vijiji. Njia hii inatumika kwa kuwa ni rahisi kuwafikia walengwa wengi katika sehemu ambazo utamaduni wa kujisomea na upatikanaji wa njia nyingine za mawasiliano una changamoto. Ili kuhakikisha upatikanaji mzuri, Stawisha Maisha hurushwa katika vituo vya redio za jamii mikoa ya Mbeya, Dodoma, Ruvuma, Rukwa, na Geita, na pia hupeperushwa kitaifa kupitia Radio Free Africa (RFA).
Kwa jamii zilizopo maeneo ya mbali yenye usikivu dhaifu wa redio, TASAF imeanzisha ubunifu wa kugawa kadi za SD zilizowekwa vipindi vya Stawisha Maisha. Kadi hizi huchezwa kwa kutumia Digital Audio Players (DAPs) katika Wilaya za Nkasi (Rukwa) na Nyasa na Namtumbo (Ruvuma), kuhakikisha hata vijiji vya mbali vinaweza kifikiwa na kipindi hiki.
Msingi wa Stawisha Maisha ni kuweuzesha walengwa kusikiliza kipindi kwa pamoja na kuwa na uelewa wa pamoja wa maudhui. Kila kipindi kina mfululizo wa michezo wa redio unaoakisi changamoto za kila siku zinazohusu lishe ya mama na mtoto na kinga ya kijamii. Baada ya michezo huo, wasikilizaji huombwa kujadili maswali fulani, kujadiliana majibu kwa pamoja, na kisha kutuma majibu yao kupitia arafa (ujumbe mfupi wa simu) kwa maafisa wa TASAF. Njia hii ya ushirikiano haina tu nia ya kujenga uelewa bali pia huimarisha umiliki na kujiamini kwa wasikilizaji.
Lengo la kipindi hiki ni zaidi ya kutoa taarifa. Hutoa taswira ya sera na mipango ya Seirkali inayoeleweka kwa wananchi ambayo zamani ilikuwa inaonekana kama mikataba ya kiserikali na isiyohusiana na wananchi. Aisha husaidia walengwa kuelewa wakati na jinsi ya kupata msaada, kama vile michango ya pesa, na kueleza matarajio, hivyo kuwawezesha watu kushiriki kwa ujasiri zaidi katika huduma za kijamii.
“Hii si redio tu; ni uwezeshaji wa maisha,” anasema Seguna Lucas, mama wa watoto wanne kutoka kijiji cha Ndondo. Kabla ya kipindi hiki, walengwa wengi hawakuwa wakipata taarifa kwa wakati kuhusu mipango ya Serikali. Sasa, jamii zinahisi kuwa na taarifa na ni sehemu ya kitu kikubwa — juhudi za kitaifa za kuboresha maisha.
Stawisha Maisha pia ina mchango muhimu katika elimu ya lishe, ikilenga mbinu za ulaji wa watoto wachanga na wadogo na afya ya mama, maeneo muhimu kwa maendeleo ya muda mrefu ya rasilimali watu. Kwa kujenga uelewa na kujiamini, kipindi hiki kiniasaidia maendeleo ya afya ya mtoto, ambalo ni jambo la msingi kupambana na umasikini.
Kusikiliza Stawisha Maisha kumegeuka kuwa shughuli ya pamoja ya kijamii inayovuka mipaka ya umri na jinsi. Makundi ya wasikilizaji hukutana katika ofisi za vijiji, na viwanja vya wazi kushirikishana hadithi walizozisikia redioni na kujifunza kwa pamoja. Hali hii huimarisha mshikamano wa kijamii na kusambaza ujumbe wa kipindi kwa ufanisi zaidi.
Prisca Yusuf, Mratibu wa Stawisha Maisha TASAF, anasema kuwa kukutana na watu “mahali walipo — ana kwa ana na kuingana na tamaduni zao” ni muhimu katika kujenga uwajibikaji. Kurusha vipindi kwa lugha za inayoeleweka vema, kwenye vituo vya redio vya jamii vinavyoaminika, na kutoa maudhui yanayolingana na maisha ya watu hufanya kipindi kuwa na matokeo mazuri zaidi.
Kipindi hiki pia kinakuza uwazi na uwajibikaji kwa kupunguza upotoshaji, uenezaji wa taarifa zisizo rasmi, na kuboresha utoaji huduma kwa wengine walengwa na wasio walengwa wa TASAF. Kwa kutoa taarifa wazi, sahihi, na kwa wakati, huimarisha uhusiano kati ya wananchi na Serikali, kuhakikisha mipango ya ulinzi wa kijamii inawafikia walengwa.
Mafanikio ya Stawisha Maisha yanadhihirisha falsafa pana ya TASAF kwamba kupunguza umasikini kunapaswa kuanzishwa kwa kuwawezesha watu binafsi kwa maarifa, kujiamini, na fursa za kujikomboa. Msisitizo wa kipindi hiki juu ya mawasiliano ya ushirikishwaji unaonyesha jinsi maendeleo endelevu yanavyopatikana watu wanaposhiriki kikamilifu katika kujenga maisha yao ya baadaye.
Stawisha Maisha itaendelea na msimu wake wa kwanza hadi Oktoba 2025, na mipango ipo ya kueneza kipindi sehemu nyingie zaidi, kuingiza sauti za vijana, na kuongeza ushirikiano tayari ipo. Lengo ni kuendeleza mpango huu ili ubaki kuwa wa maana, wenye nguvu, na wenye athari.