Habari
Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutembelea Miradi ya TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Arusha na Karatu

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas pamoja na wananchi wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas pamoja na wananchi wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo
Baadhi ya Wananchi ya Kijiji cha Oldonyowas wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo akiwaongoza wajumbe wa kamati
yake kujionea bidhaa zinazozalishwa na walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Oldonyowas
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Bi. Grace Naftal Makema akitoa maelezo ya utekelezaji wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa (aliyesimama katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Sekondari ya Oldonyowas
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Laja wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya TASAF wilayani Karatu
Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Abbas J. Kayanda akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Laja wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati hiyo (hayupo pichani)wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya TASAF wilayani Karatu
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Abdallah Chaurembo walipotembelea kivuko kilichojengwa chini ya utekelezaji wa Miradi ya Ajira za Muda katika Kijiji cha Laja Wilayani Karatu
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakikagua kivuko kilichojengwa chini ya utekelezaji wa Miradi ya Ajira za Muda katika Kijiji cha Laja Wilayani Karatu