Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

TASAF yawapa tabasamu wagonjwa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road


Katika muendelezo wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, wiki hii, Meneja Rasilimali Watu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF Bi Mariam Al-jabiri akiwa ameambatana na baadhi ya watumishi, walikabidhi msaada wa kuwalipia matibabu pamoja na vifaa tiba kwa wagonjwa wanaopatiwa huduma katika Taasisi ya Saratani Ocean Road jijini Dar es Salaam.

Bi Mariam alikabidhi msaada huo  kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Shedrack Mziray, na kueleza kwamba tulio hili limefanyikaikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, sambamba na kutambua na kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha upatikanaji wahuduma za afya.

Watumishi wa TASAF wakiwasili katika Taasisi ya Saratani Ocean Road na kupokelewa na uongozi wa taasisi hiyo

“Lengo letu la kuwa hapa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake kwa kusaidia wagonjwa mbalimbali katika hospitali hii kwa kuwapa mahitaji muhumu kama dawa na vifaa tiba,” alisema.

Alisema msaada hu unalenga kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuboresha huduma za afya na kuokoa maisha ya watanzania ambao  wenye maradhi.

Mariam ambaye ameambatana na baadhi ya wafanyakazi wa TASAF amesema Serikali imewekeza nguvu kubwa katika utoaji wa huduma za afya nchini.

Watumishi wa TASAF pia walipata wasaa wa kuwajulia hali wagonjwa hospitalini hapo huku wakiwafariji kwa kuwatia moyo na kufanya sala fupi kuwaombea uponyaji wa haraka.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Diwani Msemo ameishukuru TASAF kwa kujitoa na kusaidia wahitaji wanaopatiwa huduma katika taasisi hiyo.