Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

TASAF yashiriki mbio za Kili Marathon 2026


Watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) walikuwa ni miongoni mwa washiriki wa mbio za Kili Marathon zilizofanyika Tarehe 22 Machi, 2026 Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Ushiriki huo unaonesha dhamira thabiti ya kujihusisha na jamii katika kuimarisha afya, mshikamano na kuleta maendeleo ya taifa. Pia tunadhihirisha azma ya kuendelea kushiriki katika kuunga mkono matukio yanayohamasisha umoja na ustawi wa kijamii nchini kote.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Shedrack Mziray alishiriki kikamilifu kwenye mbio za Kili Marathon 2026, ambapo alikimbia kilometa 21.  

Katika mbio hizo, watumishi wa TASAF waliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Shedrack Mziray, ambaye aliungana na washiriki wakati wa mbio hizo.  Uwepo wake ulionesha ushiriki hai wa TASAF pamoja na kuhamasisha watumishi kushiriki katika matukio ya kitaifa ya michezo na kijamii.

Mziray ameendelea kuwa kinara wa kuhamasisha utamaduni wa kufanya mazoezi kwa watumishi, akisisitiza umuhimu wa kuwa na afya njema kwa ustawi binafsi na ufanisi kazini.

Baadhi ya watumishi wa TASAF walioshiriki kwenye mbio za Kili Marathon 2026.

Kupitia ushiriki huu, TASAF imedhihirisha dhamira ya kukuza utamaduni wa ushirikiano, afya njema na uwajibikaji wa kijamii sambamba na kuunga mkono mipango na juhudi mbalimnbali zinazowaunganisha wananchi kwa lengo moja la pamoja.