Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

Kamati ya Uongozi TASAF yafanya kikao cha kwanza


Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya TASAF Taifa, Peter Ilomo kabla ya kuanza kwa kikao cha kwanza cha Kamati hiyo jijini Dodoma, Oktoba 20, 2022

Kamati ya Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) imekutana kwa mara ya kwanza tangu izunduliwe jijini Dodoma Chini ya Uenyekiti wa Bwana Peter Ilomo. Kamati hiyo ilizinduliwa Oktoba 24, 2022 na Waziri wa Nchi (Ofisi ya Rais) Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama.

Bw. Ilomo anaungana na wajumbe wengine kwenye Kamati hiyo ambao ni Dkt. Grace Magembe, Dkt Charles Mwamaja, Dkt. Naftali Ng’ondi, Dkt. Ruth Lugwisha, Balozi Zuhura Bundala, Eng. Hussein Mativila, Adv. Richard Shilamba na Bwana Ali Salim Matta. Mkurugenzi wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga ni Katibu wa Bodi.

Kamati ya Uongozi ya Kitaifa katika kikao chake kwa kwanza