the minutes and a sub-counter with the seconds. It is made of solid gold, but also their special styles bring a new echo to public and review modern ladies watches design. www.paneraireplica.co hublot replicas watches rolex deepsea replica The white lacquered dial in the upper right quarter of the watch features a blue minute track on the outside and printed roman numerals in black all around. replica iwcs breguet replica The Maurice Lacroix logo at 12 oclock is crisp and adds a finishing touch to the small dial. Just below the main dial is a small seconds indicator with another one of those bulky looking hands.

TASAF | Habari
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Ikulu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii

Habari

TASAF: Ushirikishwaji wa Kunusuru Kaya za Walengwa utahusisha Nchi nzima Bara na Visiwani


Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Ladislaus Mwamanga akizungmza katika mkutano wa Kikao kazi cha wadau kwa ajili ya kupokea maoni kuhusu ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa uliofanyika kwenye ofisi za TASAF jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Aprili 13, 2023

Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Ladislaus Mwamanga amesema  lengo kubwa la TASAF ni kuhakikisha ushirikishwaji kaya za watu wenye ulemavu kwenye mpango wa kunusuru kaya za walengwa unahusisha nchi nzima Tanzania Bara na Zanzibar ili kukwamua kaya hizo katika lindi laumasikini

Akizungumza kwenye mkutano wa Kikao kazi Cha wadau kwa ajili ya kupokea maoni kuhusu ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu kwenye mpango wa kunusuru kaya za walengwa amesema lengola kikao hicho ni kupokea maoni kuhusu ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu kwenye mpango wa kunusuru kaya za walengwa.

“Serikali kupitia mpango huu imeamua kutoa ruzuku Maalumu kwa kaya za watu  wenye ulemavu Ili kuwaongezea uwezo wa kufanya majukumu yao,”. Amesema Ladslaus Mwamanga.

kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Watu wenye ulemavu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Suzana Mayengo amsema ujumuishaji na uimarishaji kwa watu wenye ulemavu utaliwezesha kundi hilo kupata maendeleo na kuondokana na umasikini

Ameutaka mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kuhakikisha inajumuisha na kuimarisha kaya za watu wenye ulemavu Ili kuwezesha kundi hilo kupata maendeleo

Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa awamu ya Sita Dkt. Samia Suluhu Hassan Iko mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wake wanaondokana na umasikini sambamba na kushiriki Shughuli mbalimbali za maendeleo

Naye Mwenyekiti wa Shirikusho la Vyama Vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania Ernest Kimaya ameshukuru serikali kwa kushirikisha watu wenye ulemavu kwenye mpango huu ambapo kwa sasa kundi hilo limekuwa likiweza kutoa mchango kwa familia zao

Hata hivyo ameionba serikali kuangalia namna ya kusaidia kundi la watu wenye ulemavu kwenye nafasi za ajira pindi fursa zinapopatikana

Kaimu Mkurugenzi - Huduma kwa watu wenye ulemavu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Suzana Mayengo akitoa maelezo mafupi ya Mipango na Wajibu wa Serikali kwa watu wenye ulemavu katika ukumbi wa mikutano Ofisi za TASAF Dar es Salaam

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la watu wenye ulemeavu – Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar Bw. Ussy Khamis Debe akizungumza na wadau kuhusu ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu (hawapo pichani) katika ukumbi wa mikutano Ofisi za TASAF Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wawezeshaji kutoka Mamlaka ya Maeneo ya Utekelezaji katika ukumbi wa mikutano Ofisi za TASAF Dar es Salaam