Habari
Ziara ya Mafunzo kwa Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi ya Viongozi Wakuu wa Kitaifa Zanzibar katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bw. Shauri Selenda akikaribisha wajumbe wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia ofisi ya viongozi wakuu wa kitaifa Zanzibar katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo
Mratibu wa TASAF Bagamoyo Bw. Jalala Sammatta akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa ngazi ya Halmashauri
Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia ofisi ya viongozi wakuu wa kitaifa Zanzibar Mhe. Machano Othman Said (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo
Mratibu wa TASAF Bagamoyo Bw. Jalala Sammatta akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia ofisi ya viongozi wakuu wa kitaifa Zanzibar kuhusu mradi wa kutengeneza matofali katika Shule ya Msingi Mwanamakupa kijiji cha Dunda Wilayani Bagamoyo
Wajumbe wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia ofisi ya viongozi wakuu wa kitaifa Zanzibar wakiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na kikundi cha kuweka na kuwekeza cha Tupendane katika Kijiji cha Dunda Wilayani Bagamoyo
Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia ofisi ya viongozi wakuu wa kitaifa Zanzibar Mhe. Machano Othman Said akizungumza na walengwa wa Mpango wa TASAF katika Kijiji cha Dunda Wilayani Bagamoyo
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Halima Okash akizungumza na walengwa wa Mpango wa TASAF katika Kijiji cha Dunda Wilayani Bagamoyo
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Shedrack Mziray akizungumza na walengwa wa Mpango wa TASAF katika Kijiji cha Dunda Wilayani Bagamoyo